Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

Wednesday, September 25, 2013

Wadau wamtabiria makubwa Miss Tanzania


Ni Happiness Watimanywa, alitangazwa juzi kuwa mshindi wa taji hilo baada ya safari ndefu ya kuanzia ngazi ya vitongoji, m
koa na kanda.

Dar es Salaam. Juzi katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, kamati ya shindano kubwa la urembo lenye sura ya Kitaifa, linalojulikana kwa jina la Redd’s Miss Tanzania 2013, lilimtawaza Happiness Watimanywa kuwa mshindi wa taji hilo baada ya safari ndefu ya kuanzia ngazi ya vitongoji, mkoa, na kanda.

Wadau wengi wa masuala ya urembo wanamtabiri Happiness Watimanywa kwamba huenda ataifikisha mbali Tanzania katika medani ya urembo kutokana na uelewa wake na jinsi anavyoweza kujieleza kwa ufasaha, pia kutokana na upeo alionao katika masuala ya kimataifa.

Katika mahojiano na gazeti hili baada ya shindano hilo, wadau mbalimbali wa burudani wameonyesha imani na msichana huyo anayeonekana kuwa na umri mdogo lakini mwenye upeo wa hali ya juu.

Sospeter Gerald, mbunifu wa mavazi na mtaalamu wa urembo kutoka Kenya ambaye amekuwa akifuatilia historia ya Tanzania katika masuala ya urembo kwa muda mrefu ameliambia gazeti hili kwamba safari hii, wanaweza kufika mbali kutokana na mwakilishi wao kuonekana kuwa na uwezo katika kujieleza na mwonekano pia.

Naye Alice Mutalemwa, ambaye ni mwanamitindo, aliliambia gazeti hili  kwamba Hapinness, anahitaji tu kukaa na dada mwenye hekima, amwelekeze njia, kutokana na umri wake na majaribu yaliyomo kwenye tasnia, lakini kwa jinsi alivyoonekana, anaweza kufika mbali.

Kumbukumbu za masuala ya elimu ya kimataifa zinamkumbuka binti huyo mwenye umri wa miaka 19, ni mzaliwa wa familia ya Louis Roussos ya Morogoro, amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar es Salaam, ambapo akiwa hapo, aliwahi kwenda China na Korea kusini akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbalimbali ya elimu na michezo.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza anasomea digrii ya Biashara.Kipindi ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu, alipata wakati mgumu wa kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.

Tuesday, September 24, 2013

Mtunisi: Wasanii waache ubaguzi


Msanii wa filamu nchini, Nice Mohamed ‘Mtunisi’, amesema baadhi ya wasanii wa filamu nchini, wana tabia ya kubagua wenzao katika kila shughuli zinazohitaji umoja wao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mtunisi alisema tabia hiyo itajenga chuki na kupunguza idadi ya wasanii kuhudhuria vikao na shughuli zinazohitaji umoja wao ili zifanikiwe.

“Siku hizi hakuna upendo wala ushirikiano kati yetu wasanii, wengi wana ubinafsi na hawajali wenzao, kwa mtindo huu hatuwezi kufikia mafanikio. Inatupasa tushirikiane kwa upendo wa kweli na si unafiki,’’ alisema Mtunisi.

Chidumule aukosoa muziki wa dansi


Mwanamuziki mkongwe nchini, Cosmas Chidumule, amesema muziki wa dansi hauna nidhamu na ndiyo maana ameamua kuachana nao baada ya kuokoka ili amrudie Mungu.

Chidumule aliyasema hayo hivi karibuni, jijini Dar es Salaam, kuwa mara nyingi wanamuziki wa dansi na wengineo thamani yao inakuwa ndogo mbele ya hadhira.

Alisema wengineo hufika mbali kwa kuamua kuwatuza waimbaji bangi au vitu vingine visivyokuwa na manufaa katika maisha yao, jambo ambalo ameamua kuachana nalo.

“Huu ni wakati wa kumrudia Mungu, maana si mara zote waimbaji wanakuwa na thamani kwa mashabiki wao na ndiyo maana baadhi yao wanatunzwa bangi,” alisema.