Matukio ya vurugu, kauli kinzani na hata mgawanyiko wa ndani na nje wa chama na vyama kuhusu Katiba mpya, sasa umezaa mpasuko mkubwa ambao kama hautazibwa, unaweza kuzima ndoto ya kupatikana kwa chombo hicho kabla ya mwaka 2015.
Wakati mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ukishudiwa sasa kutokana na hatua ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, ndani ya vyama vya siasa nako kumeonekana kuwapo kwa mgawanyiko wa kimtazamo, hasa kuhusu kipengele cha serikali tatu, kilivyopendekezwa kwenye Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Kabla ya uelekeo wa upepo wa sasa ambao umechukua sura ya upinzani wa vyama vya upinzani (Chadema, CUF na NCCR Mageuzi) Vs Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndani ya vyama vya CCM, Chadema na CUF tayari kulikuwa na mgawanyiko uliotokana na kuwapo kwa mitizamo tofauti kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya na pia kipengele hicho cha serikali tatu.
Wakati CCM na CUF wakivurugwa na kipengele cha serikali tatu, Chadema wao walikuwa wakikabiliwa na mtihani wa mwakilishi wao kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesigwa Baregu, ambaye aligomea agizo la chama chake lililomtaka ajiengue katika Tume hiyo kutokana na kutoridhishwa na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya.
Kwa upande wa CCM, wakati Mwenyekiti wa Chama hicho, Jakaya Kikwete akiwataka wanachama wake wajiandae kisaikolojia kuhusu suala la muundo wa serikali tatu, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, amekuwa akisisitiza sera yao ya kuamini katika mfumo wa serikali mbili.
Vivyo hivyo kwa Chama cha Wananchi (CUF), wakati Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, akiunga mkono mfumo wa serikali tatu, licha ya kusisitiza kama ni msimamo wa pamoja wa chama, lakini zipo taarifa zinazodai kuwa baadhi ya viongozi wenzake wa upande wa Zanzibar wamekuwa wakishinikiza mfumo wa serikali ya mkataba.

0 comments:
Post a Comment